Komandanti wa Shule ya Polisi Tanzania Moshi, SACP Ramadhani Athumani Mungi, amesema Shule hiyo itawajenga wanafunzi wa mafunzo ya awali kwa Maafisa uchunguzi TAKUKURU kinidhamu, uzalendo na utii wa Sheria za Nchi.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika Leo tarehe 08.10.2026 katika Shule ya Polisi Tanzania - Moshi, SACP Mungi amesema Shule hiyo imejipanga kuwaandaa Maafisa hao, ili watakapohitimu mafunzo yao wawe na uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, itakumbukwa kwamba mafunzo hayo ya Maafisa uchunguzi yanaendeshwa Shuleni hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania.