Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala Bora, Mh. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb), amefika Shule ya Polisi Tanzania Moshi Kwa lengo la kufanya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya awali kwa Maafisa uchunguzi TAKUKURU.
MH. Kikwete amesifia Mazingira rafiki na tulivu ya Shule ya Polisi Tanzania Moshi kwa KUJIFUNZIA ambapo amewataka Maafisa wanafunzi hao kuzingatia mafunzo yatakayotolewa ili wakatende Kwa weledi.
Aidha, ameipongeza Taasisi hiyo ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU kwa kazi kubwa inayoifanya.