Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi leo tarehe 01 Julai 2026 imefanya kikao cha Kamati ya Pamoja ya Kiufundi (Joint Technical Committee) kwa ajili ya kujadili uendeshaji wa programu za masomo zinazotekelezwa kwa ushirikiano kati ya TPS-Moshi na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Kikao hicho kiliongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) upande wa Taaluma, Tafiti na Ushauri, Dkt. Gles Temba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Wajumbe kutoka taasisi zote mbili walijadili maendeleo ya programu hizo na kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano ili kuongeza ubora wa utoaji wa mafunzo.