April 24, 2026
•
1 min read
Kwa niaba ya Commandant wa Tanzania Police School - Moshi, SACP Ramadhani A. Mungi, leo tarehe 24 Aprili 2026, SSP Damazo ambaye ni Adjutant wa TPS Moshi, amefunga rasmi mafunzo ya ulinzi wa viongozi maalum (VIP) kwa wanafunzi kutoka BoT Akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji, SSP Damazo amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya BoT na Tanzania Police School - Moshi. akieleza kuwa ushirikiano huo umeendelea kuimarisha utoaji wa mafunzo mbalimbali yenye tija kwa taasisi zote mbili. Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 20 Aprili 2026 na kuhitimishwa leo tarehe 24 Aprili 2026, yakilenga kuwajengea washiriki uwezo na ujuzi wa kitaalamu katika masuala ya ulinzi wa viongozi maalum. Aidha, SSP Damazo amewataka wahitimu kutumia ipasavyo mafunzo waliyoyapata kwa kuzingatia weledi, nidhamu na uzalendo, pamoja na kuiwakilisha vyema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani na nje ya nchi. Vilevile, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kutekeleza majukumu yao.