CP TATU AWAHIMIZA WAHITIMU WA UONGOZI MDOGO WA JESHI LA POLISI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII

February 27, 2026 1 min read
Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi mdogo ndani ya Jeshi la Polisi wamehimizwa kuendelea kudumisha Ushirikiano dhidi ya jamii kwani ni nguzo muhimu katika kufanikisha falsafa ya Polisi Jamii na kudhibiti uhalifu. Hayo yamesemwa na Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu Kamishna wa Polisi Tatu Rashid Jumbe Leo tarehe 27/2/2026 wakati akifunga mafunzo ya Uongozi mdogo ndani ya Jeshi la Polisi cheo cha koplo na Sajinj kozi namba 1 2025/2026 Shule ya Polisi Tanzania Moshi. Pia ameongeza kuwa askari hao wahitimu wanapaswa kutumia vizuri nafasi waliyopewa ya kufanya kazi karibu na wananchi, akieleza kuwa hali hiyo itasaidia kujenga uaminifu na kufungua fursa za kiuchumi kulingana na mazingira ya maeneo wanayohudumia