EGA YATOA ELIMU YA USIMAMIZI WA MIFUMO YA TEHAMA TPS-MOSHI

November 8, 2025 · Tps Moshi • 1 min read
Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imetoa mafunzo ya kusimamia usalama wa mifumo ya TEHAMA serikalini kwa Maafisa, Wakaguzi na Askari wa ngazi ya kawaida katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi (TPS) Ambapo lengo la mafunzo hayo ni kulinda na kutuma taarifa muhimu, kukinga taarifa zisitumike bila idhini, kulinda taswira na kupima uhimilivu wa mifumo pamoja na kupendekeza teknolojia sahihi pasipo na gharama kwa taasisi.